Alhamisi, 17 Machi 2016

ALICHOKISEMA MKUU WA MKOA WA MBEYA

MKUU wa mkoa waMbeya, Amos Makala, amekabidhiwa rasmi ofisi yake leo na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Abbas Kandoro, huku akitoa maagizo manne mazito kwa watumishi wa serikali .Makala alisema kuwa, wakuu wote wa wilaya na wakuu wa idara katika Halmashauri za wilaya zilizopo mkoa wa Mbeya, kila siku ya Alhamisi kuanzia saa nne mpaka saa nane mchana ni marufuku kukaa ofisini bali wanatakiwa kwenda kupokea kero za wananchi vijijini nakuzishughulikia. “Mimi sijaja kutengua torati bali kutimiliza. Kila mmoja wetu atimize wajibu wake na kuacha vyeo vya uadmin wa magroup kwenye Whats App na facebook” alisema Makala.
Alisema agizo lingine hataki kusikia masuala ya ugonjwa wa kipindupindu katika Halmashauri za mkoawa Mbeya, huku akiagiza kuwa lazima mazingira yawekwe safi.

Kuhusu watumishi hewa wanaolipwa mishahara alisema jambo hilo halihitaji digrii ili kuelewa na
kulitekeleza ndani ya siku 15 kama lilivyo agizo la Rais Dkt. John Magufuli, hivyo Wakurugenzi na
maafisa utumishi wameagizwa kuwabaini haraka. “Nimekabidhiwa taarifa hapa na Mkuu wa mkoamstaafu kaka yangu Abbas Kandoro, najua kuna taarifa za upungufu wa madawati katika wilaya zetu, hivyo basi kila Mkurugenzi wa wilaya akaandike barua kuthibitisha alichopeleka kwenye taarifa yake na wala msidanganye na kuogopa kueleza ukweli ili wakati wanataka kunishughulikia mimi barua zenu ziwe ushahidi kuwa mlidanganya” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Aliwaeleza kuwa yeye kwa umri wake siyo mtu wa kukaa ofisini na kauli mbiu yake ni kwamba walipo wananchi, palipo na kero naye yupo na kwa sasa chini ya serikali ya awamu ya tano wanacheza mchezo uitwao usiniguse.
Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro, alisema kuwa anawashukuru sana marais wote wa Tanzania kwa kufanya kazi nao na sasa anastaafu akiwa na miaka 66 ambapo ametumikia taifa hili kwa miaka 40.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni