Jumamosi, 5 Novemba 2016

NTONZO SEKONDARI KWA MAENDELEO BORA YA ELIMU


Mwonekano wa mwanzo wa jengo la utawala

MOTTO: “EDUCATION WITH SCIENCE TO MATCH THE GLOBAL CHANGES”
MKURUGENZI MTENDAJI WA NTONZO SEKONDARI NDUGU MASHAKA MAHINYA ANAPENDA KUWATANGAZIA WADAU WOTE WA ELIMU NA WAPENDA MAENDELEO YA ELIMU KUWA BADO ANAENDELEA KUPOKEA WANAFUNZI WANAOTEGEMEA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA PILI NA CHA TATU KWA MWAKA WA MASOMO 2018-2021, NA MITIHANI YA USAHILI/INTERVIEW INAENDELEA KILA JUMAMOSI YA MWEZI WA 10 HADI MWEZI WA 12 SHULENI NTONZO SEKONDARI.
nembo ya sekondari Ntonzo

NTONZO SECONDARY IMESAJILIWA KWA NAMBA S.4937
SHULE IMESAJILIWA NA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNONOLOJIA NA UFUNDI (WESTU) KWA NAMBA S.4937
MAHALI SHULE ILIPO
kibao cha shule ya sekondari ntonzo

Shule ipo barabara kuu iendayo tukuyu (NTANGANO) - Nje kidogo  ya jiji la MBEYA KM 5 kutoka stendi ya Uyole
AINA YA SHULE
NI YA MCHANGANYIKO WA WAVULANA NA WASICHANA, KUTWA NA BWENI NA NI KWA DINI ZOTE.
wanafunzi wakiwa katika jengo la utawala
 
wanafunzi wa sekondari ntonzo
MAZINGIRA
Ni mazuri na ya kuvutia kwa kufundishia na kujifunzia
wanafunzi wakiwa darasani wanasoma


wanafunzi wakiwa nje ya madarasa ntonzo sekondari

wanafunzi wakiwa katika moja ya mazingira ya shule

wanafunzi wakiwa katika mazingira ya shule
pia shule ya sekondari ntonzo ina mabweni ya kisasa ya wavulana na wasichana

bweni la wasichana

bweni la wavulana

HUDUMA MUHIMU; maji,umeme, mawasiliano na barabara.

mwonekano wa mbele wa jengo la utawala Ntozo sekondari



mwonekano wa kati wa shule ya sekondari ntonzo

MCHEPUO
ART (SANAA), SAYANSI NA BIASHARA

MAABARA ZOTE TATU ZIPO NA ZINA VIFAA VYA KUTOSHA


wanafunzi na mwalimu wakifanya jaribio katika maabara ya physics

wanafunzi na mwalimu wakifanya jaribio katika maabara ya biology

wanafunzi wakifanya majaribio katika maabara ya chemistry

mwanafunzi akifanya jaribio katika maabara ya chemistry

(PIA MAKTABA IPO NA INA VITABU VYA KUTOSHA)
baadhi ya vitabu katika maabara




ADA YA SHULE
ADA NI NAFUU SANA AMBAYO MWANANCHI YEYOTE WA KAWAIDA ANAWEZA KUIMUDU NA INALIPWA KWA AWAMU NNE
KUTWA-800,000/=, HOSTEL-1600000/=

JANUARI
APRILI
JULAI
OCTOBA
JUMLA
KUTWA
200,000/=
200,000/=
200,000/=
200,000/=
800,000/=
BWENI
400,000/=
400,000/=
400,000/=
400,000/=
1600000/=
WALIMU
Wapo wenye uzoefu wa masomo yote
walimu na wafanyakazi wengine wa Ntonzo sekondari

MASOMO YANAYOFUNDISHWA SHULENI
Civics, history, geography, Kiswahili, English language, physics, chemistry, biology, basic mathematics, commerce, book keeping, additional mathematics, literature in English and computer
 MAHALI FOMU ZINAPOPATIKANA
FOMU ZA KUJIUNGA NA NTONZO SEKONDARI ZINAPATIKANA MAENEO YAFUATAYO;
  • SHULENI NTONZO SEKONDARI, 
  • ZUNYA ENTERPRISES –UYOLE,
  • STATIONARY KWA MAMA KOMBE- UYOLE
  •  AGRO-SIMEX –SOWETO MBEYA
  • TUNDUMA HOTEL- MOMBA
  • SANTONA GENERAL ENTERPRISES STAND KUU- IRINGA
  • MAHINYA BROTHERS CO.Ltd- SUMBAWANGA
  • MERU SEED.Co.Ltd- MAKAMBAKO


Kwa mawasiliano: 0762 719759
                               0768 504156
                               0767 276864
                               0752645660.
                               0789189459.
Email: info@digicom.co.tz
Website: www.ntonzo.ac.tz

Jumapili, 11 Septemba 2016

KARIBU NTONZO SEKONDARI KWA ELIMU BORA YA MWANAO...



          NTONZO SECONDARY SCHOOL
                     UYOLE-MBEYA


MOTO: “EDUCATION WITH SCIENCE TO MATCH THE GLOBAL CHANGES”

NTONZO SECONDARY IMESAJILIWA KWA NAMBA S.4937

 SHULE YA SEKONDARI NTONZO

IMESAJILIWA NA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI, TEKNONOLOJIA NA UFUNDI (WESTU) KWA NAMBA S.4937


MAHALI SHULE ILIPO
Shule ipo barabara kuu iendayo tukuyu (NTANGANO)- Nje kidogo  ya jiji la MBEYA KM 5 kutoka stendi ya Uyole


AINA YA SHULE
NI YA MCHANGANYIKO WA WAVULANA NA WASICHANA, KUTWA NA BWENI NA NI KWA DINI ZOTE.

MAZINGIRA
Ni mazuri na ya kuvutia kwa kufundishia na kujifunzia

HUDUMA MUHIMU; maji,umeme, mawasiliano na barabara.












MCHEPUO
ART (SANAA), SAYANSI NA BIASHARA
MAABARA ZOTE TATU ZIPO NA ZINA VIFAA VYA KUTOSHA
(PIA MAKTABA IPO NA INA VITABU VYA KUTOSHA)




ADA YA SHULE
ADA NI NAFUU SANA AMBAYO MWANANCHI YEYOTE WA KAWAIDA ANAWEZA KUIMUDU
MASOMO YANAYOFUNDISHWA SHULENI
Civics, history, geography, Kiswahili, English language, physics, chemistry, biology, basic mathematics, commerce, book keeping, additional mathematics, literature in English and computer

 
MTIHANI WA KUJIUNGA NA SHULE
MTIHANI UTAFANYIKA NTONZO SEKONDARI
Awammu ya kwanza: Tarehe 17/9/2016 siku ya jumamosi
Awamu ya pili: Tarehe 8/10/ 2016 siku ya jumamosi

NB. Mtihani utafanyika, utasahihishwa na kutolewa majibu siku hiyo iyo.

WALIMU
Wapo wenye uzoefu wa kutosha kwa masomo yote.

PRE-FORM ONE    Ipo kuanzia tarehe 19/9/2016.
Ada kwa bweni ni Tsh.150,000/= na Day Tsh. 60,000/= kwa miezi mitatu (3) na watakao jiunga na PRE-FORM ONE WATAPEWA OFA YA ADA MWAKANI (2017)






KWA ELIMU BORA YA MWANAO…….

Kwa mawasiliano: 0762 719759/ 0768 504156
                                 0767 276864/ 0752645660.
EMAIL: ntonzosec@gmail.com

Jumatano, 6 Aprili 2016

RAIS MAGUFULI NA RAIS WA RWANDA WAZINDUA DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi leo tarehe 06 April, 2016 kwa kutembelea nchi jirani ya Rwanda, ambapo yeye na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame wamefungua Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) na Daraja la Kimataifa la Mto Rusumo katika Mpaka wa Tanzania na Rwanda. 

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, ameingia nchini Rwanda kwa usafiri wa magari akitokea nyumbani kwake Lubambangwe, katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambako alikuwa mapumziko tangu tarehe 29 Machi, 2016. 

Katika eneo la Rusumo, Rais Magufuli na Rais Kagame kwanza wamefungua majengo ya Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani kilichopo upande wa Tanzania, kisha wakafungua daraja la mto Rusumo, na baadaye wakafungua Majengo ya Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani kilichopo upande wa Rwanda.

Mradi huu wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha utoaji wa Huduma za Mpakani cha Rusumo, umehusisha ujenzi wa majengo ya mamlaka ya Mapato katika pande zote mbili na daraja lenye urefu wa mita 80 na upana wa mita 9.5, na umegharimu shilingi Bilioni 61.4 zilizotolewa kwa ufadhili wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA. 

Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi wa mradi huo Rais Magufuli ameishukuru Japan kwa kutoa fedha za kuwezesha utekelezaji wa mradi huo na ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Rwanda kupitisha mizigo yao Tanzania kupitia mpaka huo, pamoja na kuitumia bandari ya Dar es salaam. 

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi wa Rwanda na wanajumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla, kushirikiana kibiashara kwa kutumia fursa zilizopo huku akibainisha kuwa Tanzania imeanza juhudi za kuimarisha miundombinu yake ya barabara na kujenga reli ya kati, ambayo tayari washirika 13 wameonesha nia ya kufanikisha ujenzi huo. 

Aidha, Rais Magufuli amewaonya maafisa forodha na vituo vya ukaguzi kuacha mara moja tabia ya ucheleweshaji wa upitishaji wa mizigo, na amesema serikali imeshaamua kuwa barabara ya Rusumo hadi Dar es salaam itakuwa na vituo vitatu ambavyo ni Rusahunga, Singida na Vigwaza ili magari yatumie muda wa siku 3 badala ya kutumia siku zaidi ya 10, 

Kwa upande wake Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye ameongozana na mkewe Mama Janeth Kagame, pamoja na kuishukuru Japan kwa kufadhili mradi huo amesema Tanzania na Rwanda zina kila sababu ya kushirikiana kiuchumi na ameongeza kuwa ni matumaini yake kujengwa kituo hicho kutaongeza biashara na idadi ya watu wanaovuka daraja kutoka 2,000 wa sasa hadi watu zaidi ya 15,000 kwa siku. 

Akiwa Rwanda Rais, Magufuli amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Paul Kagame na hapo Kesho Rais Magufuli atashiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji wa Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Kigali
06 April, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. 

Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka. 
 Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
 Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi  wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo